Jeremiah 48:1-6

Ujumbe Kuhusu Moabu

1 aKuhusu Moabu:

Hili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo: “Ole wake Nebo, kwa maana utaharibiwa.
Kiriathaimu utaaibishwa na kutekwa;
Misgabu itaaibishwa na kuvunjavunjwa.

2 bMoabu haitasifiwa tena;
huko Heshboni watu watafanya shauri baya la anguko lake:
‘Njooni na tuangamize taifa lile.’
Wewe nawe, ee Madmena, utanyamazishwa;
upanga utakufuatia.

3 Sikiliza kilio kutoka Horonaimu,
kilio cha maangamizi makuu na uharibifu.

4 Moabu utavunjwa,
wadogo wake watapiga kelele.

5 cWanapanda kwenda njia ya kuelekea Luhithi,
wakilia kwa uchungu wanapotembea,
kwenye njia inayoshuka kwenda Horonaimu,
kilio cha uchungu kwa ajili ya uharibifu kinasikika.

6 dKimbieni! Okoeni maisha yenu,
kuweni kama kichaka jangwani.
Copyright information for SwhKC